Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Risasi
Jumamosi, Masogange alipatwa na msala huo mara baada ya kutua katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar hivi karibuni
akitokea nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ ambapo alidakwa na polisi wa
kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya nchini kilicho chini ya Godfrey
Nzowa.
Akisimulia ishu hiyo, Masogange ambaye
umaarufu wake mkubwa ulizaliwa katika video ya Wimbo wa Masogange wa
Abednego Damian ‘Belle 9’, alisema alikamatwa na watu wa uhamiaji nchini
baada ya kuhisiwa kuwa hati yake ya kusafiria ina matatizo.
“Walinikamata baada ya kuiona hati ilikuwa
na ule msala wa awali lakini walinihoji na nikawapa majibu ambayo
yaliwaridhisha, wakaniachia.
“Hii ishu inanitesa sana lakini nashukuru
Mungu kwa kuwa nakamilisha taratibu za kuwa raia wa Afrika Kusini,
nitaishi kule,” alisema Masogange alipobanwa na Risasi Jumamosi.
Juzi wakati gazeti hili likienda mitamboni,
Masogange alikuwa kwenye Ubalozi wa Sauz nchini katika harakati za
mwisho kukamilisha taratibu za kuwa na uraia wa Afrika Kusini ambako
amesema ndiko atakapokuwa akiishi.
Julai 9, mwaka jana, Masogange alikamatwa
na madawa ambayo yalihisiwa kuwa ni ya kulevya nchini Afrika Kusini,
akashikiliwa na polisi kwa miezi kadhaa.
Septemba, mwaka jana Mahakama ya Kempton ya
jijini Johannesburg, baada uchunguzi kukamilika na kubainika kuwa
hayakuwa madawa ya kulevya bali ni kemikali zinazotengenezea madawa ya
kulevya, Masogange alitakiwa kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni),
akawa huru.
Post a Comment