Home
»
Shilole
»
SKENDO
» SHILOLE, AZINGUANA NA NUHU MZIWANDA HADI WAZICHAPA!..SOMA CHANZO HAPA
Lile
penzi lililopata ‘promo’ ya kutosha ndani ya muda mfupi kati ya
mwanamuziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’ na Nuh Mziwanda limeingia shubiri
baada ya juzikati wawili hao kuzichapa. Kisa cha wawili hao kuzibuana
kinadaiwa ni baada ya Nuh kukuta sms tata ya mwanaume kwenye simu ya
Shilole ambapo inadaiwa baada ya jamaa huyo kumtaka mchumba wake huyo
ampigie aliyetuma meseji hiyo kukawa na kusuasua.
Mwanamuziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
Chanzo chetu cha habari kilichoomba jina
lake lisichorwe gazetini kilitiririka: “Shilole na mchumba’ke walikuwa
chumbani, mara ikaingia sms kwenye simu ya Shilole.
“Nuh alipoiona alimlazimisha Shilole
ampigie jamaa aliyetuma sms na aweke ‘loud speaker’, Shilole alipoipiga
ile namba, akajichanganya kidogo licha ya kuwa, jamaa alikuwa anamjua na
wala hakuwa mpenzi wake ila ni washikaji tu.
Mwanamuziki na mpenzi wa Shilole, Nuh Mziwanda akipozi.“Kuona vile si Nuh akaanza kumpiga na hapo ndipo timbwili
lilipotokea. Wote waliumia ila Nuh ndiye aliyeumia zaidi, ilikuwa ni
vurugu kweli, baada ya ugomvi Nuh akaondoka na mfuko kama wa rambo hivi
akiwa na vitu vyake kana kwamba katimuliwa,” kilidai chanzo hicho.Baada
ya kuzipata nyeti hizo, Ijumaa lilimtafuta Nuh na alipopatikana alikiri
kutokea kwa ugomvi lakini hakuwa tayari kuuzungumzia kwa kirefu.
Shilole alipopatika alisema: “Ni kweli tukio lilitokea. Ni hivi,
aliyenitumia ile meseji ni mdau wangu, aliniambia kuwa yuko Dar
tutafutane na wala si kwa mambo ya mapenzi lakini nikashangaa Nuh
analazimisha nimpigie.
“Ile napiga naongea naye, si akanipiga kofi, hapo vurugu ikatokea.
Kimsingi sikutarajia, ni kweli nampenda lakini mimi nadhani bora kila
mmoja achukue hamsini zake.“Nilimheshimu sana, wamekuwa wakinitongoza
wanaume wengi lakini nikawa nawakatalia kwa kuwa nampenda lakini leo
anakuja kunipiga kwa mtu ambaye wala sina mpango naye. Amenikasirisha
sana, acha aende zake, unajua mapenzi hayaendi hivyo,” alisema Shilole.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa, baada ya
ugomvi huo Nuh alichukua kila kilichokuwa chake na kuondoka kwenye
nyumba aliyokuwa akiishi na Shilole kwani alikuwa ni kama kahifadhiwa.
CHANZO: GPL
Post a Comment