Kwa mujibu wa TMZ, timu ya Britney Spears imemtumia Cali Lee ujumbe wa vitisho wakimuonya asifungue mdomo wake kueleza chochote walichoongea na David Lucado kuhusu Britney Spears wakati wanachepuka.
Katika hatua nyingine, watu wa timu ya Britney wameiambia TMZ kuwa Lucado na mwimbaji huyo wamesaini makubaliano maalum kisheria ya usiri kuhusu mapenzi yao na Lee pia amebanwa.
Hata hivyo, mwanasheria wa Lee amesema kuwa mteja wake habanwi kabisa na makubaliano hayo na kwamba yuko huru kuzungumza chochote kinachomhusu.