Chris Brown kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu maisha ya yake ya Jela wakati akifanya mahojiano na Billboard.
Ameeleza kuhusu ratiba ya kila siku na alichojifunza:
Mlinzi anakuamsha, unakula. Unakaa kwenye selo yako muda mwingi, kwa kawaida masaa 24 kwa siku. Labda siku za Jumatatu unaenda nje kwenye paa unapiga simu. Ni kutengwa. Unakuwa na muda wa kufocus kwenye masuala yanayohusika, katika nini cha kufanya na nini sio cha kufanya. Kiwango cha utu uzima wangu kimekuwa pamoja na utambuzi wangu wa kipi ni muhimu.
Kutambua kuwa mimi ni binadamu kama mwingine yeyote. Mwisho wa siku, ni uzoefu mzuri. Unakuwa unaapreciate kwa vitu vingine ambavyo viko nje. Burger ina ladha mara 1,000 zaidi ukiwa nje (anacheka). Nimekuwa naapreciate vitu nilivyobarikiwa na ninavyofanya: muziki, kuwa na uwezo wa kutunza familia, kuwa na uwezo wa kuwaonda marafiki na familia.
Chris Brown asimulia maisha ya jela, ratiba ya kila siku na alichofunzwa
Na kuwa na uwezo wa kufanya nachokipenda na bado nikawa na uwezo wa kufanya katika muda ambao wengi hawafikirii, ‘Oh, sawa ameanguka,’ bado nikawa na uwezo wa kuwa na muendelezo uleule.
Akizungumzia akilichokimiss wakati akiwa jela, Chris ameeleza kuwa familia yake hasa ndio aliyokuwa akiimisi, baba, mama na ndugu zake na kuona watu wakiwa na furaha wanaomtia moyo.
Chris Brown alizungumzia pia maisha yake na Rihanna kama ipo siku uhusiano wa mapenzi kati yao utarudishwa. Amesema kuwa watu ndio hurudisha vitu hasi vya zamani na kwamba kwa kuwa anaangalia mbele, maneno ya watu sio kitu.

LAANA

 
Top