Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa hii leo kwenye gazeti la The Mirror la nchini Uingereza imeelezwa kwamba mkurugenzi huyo yupo katika ikikaango kutokana na kushindwa kufanikisha usajili wa baadhi ya wachezaji ambao walipendekezwa na meneja wa Spurs Mauricio Pochettino.
Baldini alielekezwa kufanya usajili wa mchezaji mmoja kati ya Loic Remy, Wilfried Bony ama Danny Welbeck ikiwa ni pendekezo ambalo liliaminiwa huenda lingeendelea kukiimarisha kikosi cha Spurs.
Lakini pamoja na mbinu mbali mbali kufanyika kwa ajili ya kumsajili mmoja kati ya washambuliaji hao ambao angejiunga na akina Emmanuel Adebayor pamoja na Roberto Soldado, bado suala hilo lilishindikana mpaka dirisha usajili lilipofungwa usiku wa Sepetemba mosi.
Hata hivyo inaelezwa kwamba Baldini alisita kufanya usajili wa wachezaji wengi kwa lengo la kuepuka gharama kubwa ambazo zingeifanya klabu hiyo kuingia hasara kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Katika msimu wa ligi uliopita Spurs walitumia kiasi cha paund million 110 kwa ajili ya usajili wa wachezaji, na mwishoni mwa msimu walishindwa kufikia malengo ya kuwa miongoni mwa klabu zilizomaliza katika nafasi nne za juu.