Akiongea na East Africa Radio hivi karibuni, Lady Jaydee aliutaja wimbo mpya atakaoutoa mwishoni mwa mwezi huu. “Mwezi wa kumi na moja mwishoni natoa nyimbo mpya pamoja na video. Wimbo unaitwa Forever nimemshirikisha Dabo mdogo wangu, toka mimi kuzaliwa ananifuata yeye. Yeah ni ngoma ya kwanza nilikuwa namuacha apevuke kwanza akue na ajisimamie.”
Pia kwenye ukurasa wake wa Instagram alitease mashairi ya wimbo huo.
“Haya mapenzi kweli I just can’t explain eeeeh, Utanielewa vipi iiih Moyo wangu wote uko kwako when ur not around Ur not here with me Ooooh baby i can’t breathe Unapotoka tu, usipokuwepo tu moyo wangu #Forever #JideFeatDabo#Comingsoon.”
Post a Comment