Home
»
WASANII
» Mchepuko: Inspector Haroun na Baby Madaha Wanaswa Usiku Live wakila Bata!!!!
Katika hali ya kushangaza, mastaa wawili wa muziki, Baby Madaha na
Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’ wamenaswa usiku wakila bata huku wakiwa
kimahaba.
Staa wa Bongo Fleva, Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’ akigonga busu shavuni kwa Baby Madaha.
Tukio hilo lilinaswa na kamera ya paparazi wetu hivi karibuni kwenye
pub moja iliyopo maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo awali Inspector
alionekana akiwa amemkalia Madaha huku wakipigana mabusu.
Baada ya paparazi wetu kujitokeza na
kuanza kuwafotoa, Inspector ambaye ni mume wa mtu alishituka na
kujinasua kutoka kwenye mwili wa mwanadada huyo.
Mtu mzima ‘Inspector Haroun’ na Baby Madaha wakizuga flani hivi... baada ya kuhisi uwepo wa paparazi wetu eneo la tukio.
Alipoulizwa juu ya kile alichokuwa akifanya
wakati ni mume wa mtu, Inspector alisema: “Kaka kwani kuna kibaya gani
tulichokuwa tunafanya, tupo hapa tunapanga mambo yetu ya muziki na wala
hakuna ishu zaidi.”
Kwa pamoja wawili hao wakipozi kimahaba.
Baby Madaha kwa sasa haijulikani anatoka kimapenzi na nani ila
Inspector Haroun ni mume wa Bahati ambaye alifunga naye ndoa mwaka 2004
na wamejaaliwa kupata watoto wawili ambao ni Nassir na Shadya.
Chanzo: Gpl
Tunazani ungependa kusoma hizi
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.