Mganga aliyejita-mbulisha kwa jina moja la Kimweri ameibuka na madai
mazito kuwa ndiye aliyemng’arisha staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah
Abdukareem ‘Meninah La diva’ hivyo kutoa siri nzito ambayo wengi
hawakuijua.
Staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mganga huyo amekuwa akimfanyia ndumba
msanii huyo ili arudiane na aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul
‘Diamond Platinum’.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mganga huyo amekuwa akidai kwamba, huwa
msanii huyo anatinga nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala-Komakoma
jijini Dar kisha kumlilia shida yake akimtaka afanye juu chini
kuhakikisha anamrudisha Diamond mikononi mwake.
Baada ya kukisikia chanzo hicho, waandishi wetu walikwenda nyumbani
kwa mganga huyo na walipomuuliza ishu hiyo alikiri Meninah kufika kwake
ili kufanyiwa ndumba arudiane na Diamond.
“Yule msanii anayeitwa Meninah ambaye habari zilivuma kuwa anatoka na
Diamond na kukanusha, huwa anakuja hapa kufuata tiba na kikubwa
anachokitaka anataka nimvute Diamond ili warudiane,” alisema.
Meninah alipoulizwa kuhusu madai hayo aliruka kimanga na kudai hakuwahi kuwa na uhusiano na Diamond na wala hamjui mganga huyo.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.