Akizungumza katika kikao cha hali ya uhalifu
mkoani Tanga kilichowashirikisha maofisa usalama barabarani jana,
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Fraisser Kashai, alisema tukio hilo
lilitokea juzi saa 8 usiku wakati mume wa mke huyo akiwa amelala.
Alimtaja
majeruhi huyo kuwa ni Sharif Suleiman(25) ambaye ni mfugaji alikatwa
mkono wa kushoto kwa silaha aina ya shoka na usiku huohuo mtuhumiwa
kudaiwa kutoroka kwenda kwa shangazi yake anayeishi kijiji cha Songe.
Alisema
uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini kuwa wawili hao walikuwa katika
misigano ya ndoa kwa muda mrefu na kila mmoja alikuwa akimtuhumu
mwenzake kwa kukosa uaminifu.
Kamanda Kashai alisema
majirani walisema kuwa wenza hao kila siku walikuwa wakipigana na
kutuhumiana kwa kila mmoja kumwendea mwenzake kinyume.
Post a Comment