Kamanda huyo alitoa wito huo
baada ya kutakiwa kutoa taarifa ya kukatwakatwa na panga kwa mwanamke
mmoja kutokana na kukataa kufanya tendo la ndoa na mumewe kwa sababu ya
uchovu.
Kamanda Mohamed alisema alikuwa hajapata
taarifa za kutokea tukio hilo, lakini akashauri wanawake walioolewa
kuwajibika katika masuala ya unyumba ili kupunguza migogoro ya ndoa.
Mwanamke
huyo mkazi wa Sigunga wilayani Uvinza, Jasmin Kassim alilazimika
kufanyiwa upasuaji kwenye Hospitali ya Misheni ya Heri wilayani Kasulu
kuunga mifupa ya mikono yake baada ya kushambuliwa na mumewe.
Akisimulia
mkasa huo juzi, Kassim alidai kuwa Oktoba 29 saa 4:00 usiku, baada ya
kumaliza kula chakula alikwenda chumbani kulala ndipo mumewe alipotaka
haki yake ya ndoa, lakini alimwambia kwamba alikuwa amechoka.
“Kilichonikuta
baada ya kumkatalia alitoka nje na alirudi akiwa ameshika panga, ghafla
akaanza kunipiga kisha kunikatakata katika mikono yote miwili.
“Nilipozinduka nikajikuta nipo zahanati ya kijiji, nikashonwa zaidi ya nyuzi tano,” alidai Kassim.
Kassim
alisema kutokana na majeraha hayo alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya
Maweni iliyopo Ujiji ambako alilazwa.
Baada ya uchunguzi iligundulika kuwa mifupa ya mikono imeachana na ndipo akafanyiwa upasuaji kwa mara ya pili.
Baada ya uchunguzi iligundulika kuwa mifupa ya mikono imeachana na ndipo akafanyiwa upasuaji kwa mara ya pili.
Post a Comment