Binti huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja akifanya yake.
Tukio hilo la aibu lilijiri kwenye
onesho la Kundi la Mashauzi Classic ndani ya Ukumbi wa Mango Garden,
Kinondoni jijini Dar ambapo lilikuwa likitambulisha albam yake mpya ya
Sura Surambi, Sura Siyo Roho.
...Akizidi kuserebuka ndani ya ukumbi huo.
Awali binti huyo alionekana ukumbini
humo akiwa mpole na mwenye sura ya soni huku akipata kilaji polepole
kabla ya kumkolea na kuwa staa wa kubinuka kihasarahasara na kumwaga
‘lazi’ mbele ya kadamnasi huku akiacha sehemu ya maungo yake nyeti
kweupe.
“Jamani pombe mwanaharamu. Muone yule
binti wa Kiarabu, kaja mpole lakini hebu ona vituko utadhani kuna skruu
imefunguka kichwani,” alisema mmoja wa mashuhuda.Katika hali
iliyoonekana kuzidi kuelemewa na kilaji, binti huyo alianza kuwavaa
wanamuziki stejini na kuwakumbatia kisha kuinua mguu na kurusha mateke
ya kinyumenyume kama mwanasoka, Cristino Ronaldo wa Real Madrid.
Post a Comment