0
Kuna makatazo mengi sana Korea Kaskazini. Kuanzia matangazo ya televisheni kutoka kwenye kituo cha serikali peke yake. Wananchi kutosafiri kwenda nje ya miji yao bila ruhusa maalum na pia kutomiliki biblia.


Hayo yote tisa, kumi, hairuhusiwi watoto wanaozaliwa kupewa jina Jong-un.
Jina hilo la kiongozi kijana wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, limetunzwa kwaajili yake peke yake na hivyo kuendeleza utamaduni ulioanzishwa na babu yake.
Na wananchi waliokuwa na jina hilo wakati Kim alipoingia madarakani mwaka 2011, walilazimika kuliacha.
Chanzo: NY Times

Post a Comment

 
Top