0
Kaka mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Nicholaus  amesimamia fumanizi la dada’ke ambaye ni mwanafunzi wa sekondari moja jijini Dar  ambapo alimfumania chumbani na njemba mmoja sharobaro aliyetajwa kwa jina la Abuu Ally, mkazi wa Mbagala-Charambe, Dar.

Akisimulia  mkasa  wa  fumanizi  hilo, Nicholaus alisema amekuwa akiumizwa na taarifa kwamba kila ikifika saa 2: 00 usiku kuna mwanaume amekuwa akijipenyeza na kuingia chumbani kulala na mdogo wake wa kike kisha kuchomoka alfajiri. Alidai kuwa kuwa mara nyingi vitendo hivyo hufanyika wikiendi .

Ili  kumnasa  mwanaume  huyo, Nicholaus aliandaa  vijana  kadhaa  wa  kazi  kwa  ajili  ya  fumanizi  na  kisha akamtaarifu Mjumbe wa Mtaa wa Maji-Matitu, Hawa Ally kuwa wana kazi eneo lake hivyo akatoa ushirikiano uliofanikisha kumnasa Abuu.

Baada ya kukiri kosa mbele ya kiongozi huyo wa serikali za mtaa, pande zote zilikubali kusuluhishwa ambapo Abuu alikubali kulipa faini ya shilingi laki moja na kupewa muda wa siku moja kutekeleza adhabu hiyo.
 
Credit: Ijumaa Weekenda

Post a Comment

 
Top