Msanii Deogratius Shija akizungumzia jambo |
Chanzo makini kilieleza kwamba tukio hilo lilitokea katika Mtaa wa Mchangani, Mwananyamala, Dar ambapo wakala wa Chama cha CUF walimkatalia kwamba yeye siyo mkazi wa mtaa huo hivyo hapaswi kujiandikisha hapo ambapo Shija aliendelea kuzozana nao. Paparazi wetu alimtafuta Shija ambapo alisema:
“Ni kweli nilienda kujiandikisha mawakala wakakataa nisijiandikishe kwa sababu nilishahama mtaa ambapo nilizozana nao hivyo baada ya vurugu kuzidi polisi walikuja kuniondoa hata hivyo sikujiandikisha, kura sitapiga.”
Post a Comment