0
Mtandao wa kijamii wa Instagram umetangaza rasmi kufikisha watumiaji milioni 300na hivyo kuipita kwa mbali zaidi mtandao Twitter wenye watumiaji milioni 284,akiongea kwenye kipindi cha Newsbeats mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Kevin Systrom akiri kukua zaidi kwa mtandao wake huo wa kijamii kutokana na kutumiwa zaidi na makampuni na watu binafsi kusambaza taarifa kwa kwa jamii kwa njia ya picha.Kitu kingine kinachofanya mtandao wa Instagram kukua zaidi ni baada ya kununuliwa na Facebook yenye watumiaji bilioni 1.35 mwaka 2012.Instagram uthibitisha akaunti za makampuni,watu maarufu na wanamichezo imesababisha kuifanya iweze kupendwa zaidi na watu wa rika zote kote Duniani. 


Logo ya instagram

Mkurugenzi huyo pia aelezea jinsi wanavyokabiliana na akaunti bandia kwa kuzifuta mara moja na pia kuwa na mpango wa kuanzisha kipengele kipya kwa ajili ya matukio.


Mfanao wa muonekano wa instagram

Post a Comment

 
Top