Tamrina Posh ‘Amanda’.
Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ amefunguka kwa mara ya kwanza
kuwa japokuwa wametengana na mumewe Hamisi Bwela, bado kila mmoja
anampenda mwenzake.
Akizungumza hivi karibuni, Amanda alisema, watu wengi
wanadhani alivyoachana na Hamisi, hawaivi tena kitu ambacho siyo kweli
kwani wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali.
“Sina ubaya na Hamis na wala hajawahi kunitendea vibaya kwa hiyo hata
kama nitapata tatizo wakati wowote akipata taarifa ndiyo wa kwanza
kuja, so bado tunapendana ila hatuwezi kurudiana tena,” alisema Amanda.
Post a Comment