Wakati
ambapo dunia ikiweka jitihada zote kuisaka ndege ya shirika la Malaysia
aina ya Boing 777 iliyopotea ikiwa na watu 239 wakati ikielekea Beijing, mhubiri maarufu wa Nigeria T.B Joshua ametoa utabiri kuwa ndege hiyo imezama baharini!
Jumapili
iliyopita, T.B Joshua ameeleza kanisani kwake (SCOAN) kuwa ndege hiyo
ilianguka na imezama ndani kabisa kwenye tope za bahari na kwamba hivi
karibuni vipande vya ndege hiyo vitaanza kuonekana vikielea.
“Ndege
hiyo iko ndani kabisa ya bahari. Baadhi ya vipande vitaanza kuonekana
vikielea baharini muda wowote kuanzia sasa." Alisema T.B Joshua.
“Roho
zao zipumzike kwa Amani. Tunaomba bwana azipe familia zao na wapendwa
wao nguvu/uimara kushinda upotevu huu. Maombi yetu na upendo viko nao,
nchi ya Malaysia na nchi nyingine ambazo zilikuwa na abiria katika ndege
hiyo.” Alisema T.B Joshua kwa mujibu wa mtandao wa Nigeria wa
Informationnng.
Hayo ni mambo ya imani!
Wakati
dunia ikiwa bado haijafahamu ilipo ndege hiyo, wizara ya mambo ya nje
ya China imeitaka Malaysia kuharakisha juhudi zake za kuitafuta ndege
hiyo iliyokuwa na abiria 154 raia wa China kati ya abiria 239 waliokuwa
katika ndege hiyo.
Ndege
hiyo ilipotea mwishoni mwa juma na kumekuwa na mashaka kwamba huenda ni
bomu au utekaji nyara unaweza kuwa uliiangusha ndege hiyo
Post a Comment