Muigizaji anaetajwa kuwa kati ya waigizaji bora zaidi wa kike Tanzania, Yvonne Cherryl aka Monalisa ameeleza kuwa waigizaji wa Tanzania hushindwa kung’ara wanapotajwa kuwania tuzo kubwa Afrika kwa kukosa sapoti ya Watanzania.
Nyota
huyo wa tamthilia ya Siri ya Mtungi ameeleza katika makala
iliyoandaliwa na Rahab Fred wa 100.5 Times Fm iliyokuwa ikielezea juu ya
ushindi wa wa Mkenya Lupita Nyong’o kama mfano wa kuigwa kwa waigizaji
na wadau wa filamu Tanzania.
Monalisa
alieleza kuwa Lupita amefanikisha kutokana na sapoti kubwa aliyoipata
kutoka kwa wakenya tangu awali, na kutoa mfano wake mwenyewe na
muigizaji mwenzake wa tamthilia ya ‘Siri ya Mtungi’ kuonesha jinsi
watanzania wasivyosapoti.
“Kwa
watanzania nikisema eti watu wote kwa ujumla tumpush mtu yaani hiyo
ntahubiri mpaka mwaka kesho. Kwa sababu kuna watu kibao…mimi mwenyewe
niliwahi kuwa nominated kwenye tuzo za Nigeria lakini zinafanyika New
York kila mwaka.
Nilikuwa
nominated na nilikuwa msanii wa kwanza kwa wakati huo. Niliomba kura
lakini hamna mtu ambaye alijitolea kusema kwamba labda jamani tumpigie
kura huyu ni mtanzania mwenzetu.
Lakini
wanakusubiri mpaka ufike kwenye mafanikio ndio wanaanza kusema kuwa
huyu ni wa kwetu jamani tumpigie kura.” Alisema Monalisa.
Aliongeza
kuwa ingawa tamthilia ya ‘Siri ya Mtungi’ ilikuwa nominated kwenye
vipengele 7 kwenye tuzo za AfricaMagic Viewers' Choice Awards mwaka huu,
na Juma Rajab aka Cheche akitajwa katika kipengele kimojawapo, hakuna
hata msanii mmoja aliyepost kumuombea kura.
Katika
hatua nyingine, Monalisa aliwashauri wasanii wa Tanzania wasibweteke
wanapopata nafasi ya kuingia kwenye tasnia ya filamu bali waongeze
jitihada, kusoma na kufuatilia kwa ukaribu weledi wa mambo ya filamu.
Alidai
kubweteka kunachangiwa na tabia ya baadhi ya ma-director kuangalia
uzuri wa msichana kama kigezo cha kuwapata washiriki kabla ya uwezo wa
kuigiza.
“Unajua
wasanii wa Bongo wengi wanachukuliwa labda hivi director amepita
amemuona msichana mzuri, wenyewe siku hizi wakiona msichana mzuri
wanasema ‘cast ile’. Kwa hiyo mtu anachukuliwa tu akishajiona ‘ah mimi
ni mzuri nikishavaa kimini changu hapa nauza’, basi anajibweteka hafanyi
chochote kuhusiana na kazi yake..”
Aliwashauri
wasanii wanapopata nafasi wasibweteke bali wawe na kiu ya kujifunza na
kufuatilia kwa karibu kinachoendelea katika kiwanda cha filamu.
Tamthilia
ya Siri ya Mtungi, ilitajwa kuwania vipengele saba katika tuzo za AMVCA
2014 zilizofanyika juzi jijini Lagos, Nigeria, lakini iliambulia
patupu.

Post a Comment