Utata wa muda mrefu ulioibuka baada ya kijana anaejulikana kwa jina la Brandon Howard kudai kuwa Michael Jackson ndiye baba yake mzazi, vipimo vya DNA vimeonesha kuwa huo ni ukweli kwa asilimia 99.9.
Brandon
ni mtoto wa Miki Howard, mwimbaji wa nyimbo za injili aliyekuwa rafiki
wa Michael Jackson na alikuwa akizunguka nae mara kadhaa kwenye ziara na
matamasha yake na alikuwa anawakilishwa na baba yake Michael Jackson,
Joe Jackson miaka ya 1980.
Taarifa
za vipimo vya DNA ziliwekwa wazi na daktari wa meno na upasuaji wa
Beverly Hills, Dr. Joseph Goodman alipofanya mkutano na vyombo vya
habari Alhamisi wiki hii ambapo alifungua bahasha na kusoma matokeo ya
DNA yanayoonesha kuwa Michael ni baba mzazi wa Brando kwa asilimia 99.9.
“I think we have the proof.” Alisema daktari huyo.
Hata
hivyo, chanzo kimoja kiliiambia Daily News ya Marekani na kusisitiza
kuwa Brandon sio mtoto wa Michael Jackson bali ni mtoto wa baba yake
Michael, mzee Joe Jackson.
Wakati
vuguvugu linaendelea, mwimbaji anaejulikana kwa jina la Augie Johson
amejitokeza na kudai kuwa Brandon ni mtoto wake yeye na kwamba ana
vielelezo vyote na yuko tayari kuviweka wazi na hata kuchukuliwa vipimo
vya DNA.
Michael Jackson alifariki na kuacha watoto watatu wanaofahamika ambao ni Prince Michael (16), Paris (15), na Blanket (11).
Inasemekana kuwa Brandon ndiye mtoto ambaye Michael Jackson alimuimba kwenye wimbo wake wa ‘Billie Jean’.
Baada
ya kushambuliwa na baadhi ya watu kuwa alikuwa anataka tu kupata
matunzo kama mtoto wa Michael Jackson huku mwanasheria wa Michael
akisisitiza kuwa hawajawahi kusikia hata Michael akimtaja, Brandon
aliandika kwa urefu maelezo yanayoonesha kuwa hakuwa na sababu ya
kutafuta huduma kama mtoto wa Michael Jackson kwa kuwa hata hapo alipo
anatunzwa vizuri.

Post a Comment