VIFARU
vya jeshi vilivyo katika maeneo mbalimbali ya jiji hili, vimeonyesha
kuwashitua na kuwashangaza asilimia kubwa ya wachezaji wa Yanga.Hata hivyo, Ubalozi wa Tanzania nchini hapa chini ya Balozi Mohammed Haji Hamza umewahakikishia kwamba mambo yako safi na hawapaswi kuwa na hofu.
Wachezaji wa Yanga ambao wameweka kambi nje ya jiji hilo katika hoteli maalum kwa ajili ya kambi za timu ya Nile Paradesi Inn iliyo ufukweni mwa mto Nile, wamekuwa wakizungumzia vifaru hivyo.
Lakini kilichowashangaza zaidi ni kuwa vifaru hivyo viko katika maeneo mbalimbali ya barabara na ajabu zaidi wananchi wanaona ni kitu cha kawaida.
“Unajua vifaru viko barabarani kabisa, lakini watu wanaona kawaida tu,” alisema nahodha na muuaji wa Ahly jijini Dar es Salaam, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Lakini Balozi Hamza ambaye ametoa ushirikiano mkubwa kwa Yanga tangu imewasili jijini hapa, amesema ni sehemu ya serikali ya Misri kuimarisha ulinzi.
“Hiyo ni mipango yao kuimarisha ulinzi, lakini kila kitu kinaendelea vizuri na vijana waendelee tu na maandalizi yao, hawapaswi kuwa na hofu,” alisema Balozi Hamza ambaye ni mwanamichezo.
Post a Comment