Kamanda wa kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya Godfrey Nzowa alilithibitishia Gazeti la MTANZANIA kuwepo kwa tukio hilo akiomba jina la mchungaji huyo lihifadhiwe kuepusha kuvuruga uchunguzi.
“Ni kweli tukio la aina hiyo lipo lakini watu kama hawa siwezi
kusema moja kwa moja kuwa Mchungaji ndio muhusika hadi nipate
vithibitisho vya kutosha ikiwa kuendesha kanisa kwani wengi wao
wanatumia makanisa kama mwamvuli wa kujificha na kufanya biashara
hii,”Alisema Nzowa.
Alisema kwa sasa watu hao wanashikiliwa na Jeshi hilo ambapo wawili
kati yao si raia wa hapa nchini wakati upelelezi ukiendelea kabla ya
kuweka hadharani ukweli wa mambo.
Post a Comment