Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Leonard Celestine ambaye anasomea
upadri, anayemalizia masomo ya falsafa (philosophy) mwaka wa tatu
katika Chuo cha Jordan mjini Morogoro, anadaiwa kuaibika gesti, kisa
kikiwa ni mke wa mtu gesti.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio
hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni kwenye Gesti ya Silver Inn
iliyopo maeneo ya Msamvu mjini Morogoro ambapo kijana huyo alipewa
kipondo cha aina yake na kunyang’anywa kila kitu huku akiachwa kama
alivyozaliwa na kulazimika kujisitiri na taulo la nyumba hiyo ya wageni.
Chanzo
hicho kilidai kwamba, kijana huyo ambaye ni mwenyeji wa Iringa alikuwa
na mchezo wa kutembea na huyo mke wa mtu tangu mwaka jana ambapo mumewe
aliamua kumwekea mtego ulipofyatuka akanaswa laivu.
Ilidaiwa kwamba, kama ilivyo seminari
zote za Kikatoliki, mwanafunzi hutakiwa kukaa ndani lakini Leonard
alidaiwa kuwa alikuwa akitoroka hasa siku za wikiendi au siku akiwa na
vipindi vinavyoishia asubuhi na kwenda kukutana na mke huyo wa mtu na
kujiachia naye kwani mumewe ni mtu wa kusafiri mikoani.
Ilisemekana
kuwa kutokana na kujiachia huko mwenye mke aligundua na kuanza
kumfuatilia tangu mwaka jana hadi alipowanasa hivi karibuni.
Baada ya
kunaswa, Leonard alipewa kipigo cha aina yake na watu ambao tayari
walikuwa wameshaandaliwa na mwenye ‘mali’ ambapo alilia huku akiomba
asamehewe ili yasije kuvuja akakosa upadri kwani ameshafika mbali.
Ilidaiwa kwamba, raia hao
wenye hasira walimpokonya simu, begi lake lililokuwa na madaftari na
nguo hivyo alitoka chumbani bila nguo na badala yake aliomba taulo
kujisitiri.
Credit: Gazeti la Ijumaa Wikienda/Gpl
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.