0

Kupendeza kwa mmoja kunaweza kuwashawishi wengi kujaribu kuvaa viatu hivi bila kujua kuwa vinaweza kubadilisha mwonekano wake kulingana na namna unavyoweza kuvimudu.
Kiatu hiki kinaweza kuongeza mvuto wako endapo utaweza kukimudu na kutembea na
cho kwa uhuru bila kuwa na wasiwasi wowote.
Kuweza kuhimili viatu virefu kunamfanya mvaaji kuonekana mrembo na mwenye kujiamini. Ni viatu ambavyo vinaweza
 kuonekana kwenye mazingira yoyote isipokuwa kwenye michezo.

Tofauti na aina nyingine za viatu hivi inaweza kuvaliwa na nguo yoyote iwe sketi ndefu au fupi, gauni refu na fupi, suruali za kitambaa na jeans.
Kama unajiona huwezi basi usivae kabisa kwani vinaweza kukupotezea mvuto wako na kuwa kichekesho mbele za watu kutokana na namna utakavyoonekana ukihangaika nacho.

Post a Comment

 
Top