Akipiga stori na Stori Mix, Dk. Cheni alisema amekubali kubadilisha
baadhi ya vipande vya Filamu ya Shoga kama alivyoamriwa na bodi hiyo
lakini akasema kilichofanyika kwenye sinema hiyo ilikuwa ni kuvaa
uhusika halisi wa ushoga ili jamii ijifunze. “Lengo lilikuwa kuifunza
jamii, lakini wao wameona hakuna maadili.
Nashauri wawe makini kuichunguza jamii nzima siyo tu kuangalia upande
wa filamu, wasiwe watu wa kufungia kazi zetu ili waonekane wanachapa
kazi. Kikubwa cha kutazamwa ni wazo la mtunzi na ujumbe aliotaka
kuufikisha kwa jamii,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment