0

STAA wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda amewachana wasanii ‘wanaotembea’ na mameneja wao kwani ni ujinga wa mawazo na yeye kamwe hawezi kufanya hivyo.

Staa wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda.
Akizungumza na gazeti hili, Isabela alisema katika maisha yake hajawahi kuwa na uhusiano na meneja au prodyuza na huwa anawashangaa na kuwasikitikia wasanii wanaofanya hivyo wakati siyo njia sahihi ya kujikwamua kimuziki.
“Huwezi kuchanganya kazi na mapenzi, kamwe siwezi kutoka kimapenzi na meneja wangu kwa sababu najua ufanisi wa kazi utakuwa mdogo tu,” alisema Isabela.

Post a Comment

 
Top