MAANKO mambo vipi?
Jana katika Gazeti la Ijumaa, niliandika makala kuhusu mwanafunzi mwenzenu mmoja, anaitwa Abdulaziz Chende, lakini nyinyi mnamfahamu zaidi kama Dogo Janja, yule kijana kutoka Ngarenaro pale pande za Arusha, ambaye ni msanii mwenye jina katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya.
Mtakuwa mnamfahamu, aliibuliwa na Madee, jamaa kutoka Kundi la Tip Top Connection, aliyeimba wimbo wa Pombe Yangu, ambaye anajinasibu kama Rais wa Manzese.
Si
unajua jamaa hawa walitifuana? Dogo analalamika anapunjwa mkwanja wake
wa shoo, kaka mtu anasema dogo anakula kitu cha Arusha na tena anakacha
kwenda shule, pale Makongo sekondari. Wakabishanabishana, dogo
akajiondoa Tip Top Connection akakimbilia zake Mtanashati Entertainment.
Lakini nako wameshindwana na moja ya sababu za kufukuzwa kwake, ni yale yale madai ya Madee, kwamba kijana hataki kwenda shule, kwa sababu hayo yalikuwa moja ya makubaliano yao.
Jana nimemsema sana, kwa sababu nadhani anakosea mno kukacha shule hivi sasa, kwa vile bado ana umri mdogo, ambao kama akienda vizuri, basi ana uhakika wa kuyaendesha maisha yake fresh sana kwa sababu si atakuwa na fedha ya kutosha tu kutokana na kazi zake za muziki?
Sasa baada ya kuwa nimesema naye jana kupitia safu yangu ya ZA CHEMBE LAZIMA UKAE, leo naona niwashirikishe na nyinyi, kwa sababu nina uhakika kabisa kwamba tunaweza kuwa na kitu cha kujifunza kutoka kwake, hasa katika kipindi ambacho kizazi chenu cha Dotcom, kinaishi kwa kuiga mambo sana, mengi kati ya hayo yakiwa hayana msingi katika maisha yenu ya baadaye.
Mimi nimejifunza kitu kimoja kutokana na kitendo cha Dogo Janja kukacha shule. Ustaa unamzuzua, unampa kichwa na mbaya zaidi, anafikiri kusoma ni kupoteza muda!
Lakini ninajua nyinyi maanko zangu pia wote mnapenda sana ustaa, yaani basi tu labda mmekosa fursa. Ninawaonaga baadhi yenu mkiwa mnaiga muziki wa Bongo Fleva tunapokutana kwenye daladala, yaani mnaimba mtafikiri nyimbo ni zenu.
Tena baadhi yenu mna-copy hadi zile za majuu. Ni sawa maana wakati mwingine baada ya pilikapilika nyingi za skuli tunahitaji kupumzisha akili.
Katika aina ya maisha ambayo jamii yetu inaishi, ustaa siyo kitu kizuri kwa wanafunzi. Ninajaribu kujikumbusha watoto wengi waliopata majina makubwa wakiwa na umri mdogo, sina uhakika na elimu au maisha yao ya sasa yalivyo.
Jamii yetu haitazami umri mtu anapokuwa staa, yenyewe inawachukulia kama watu wazima wenzao, hasa kwa kuwa ustaa wao mara nyingi huwa ni kuburudisha watu wazima.
Katika hali kama hiyo, ni vigumu sana kutuliza kichwa na kuwekeza katika kusoma. Fikiria kama hivi karibuni tuliripoti kuwa Dogo Janja na Dogo Aslay walivunja uchumba wa mtu huko Newala. Yaani baada ya shoo, mwanamke bila hata kujali kama wale ni watoto, eti akataka wamchukue wakalale naye!
Namkumbuka mtoto mmoja alikuwa akiigiza kipindi cha nyuma sana, aliitwa Anita, sina uhakika alipo sasa hivi. Aliigiza vizuri sana, lakini pamoja na udogo wake kiumri, alionekana katika majumba ya starehe akiwa na watu wazima.
Rai yangu kwenu ni kwamba tusipende ustaa hivi sasa tukiwa masomoni, hatutaweza kusoma. Niwaambie, unaweza kuishi vizuri na kwa uhakika sana ukiwa umeelimika, lakini ukaishi kwa shida na kubahatisha hata ukiwa maarufu kiasi gani kama kichwani mwako ni kutupu.
Sanasana utatumiwa na wajanja kuwatengenezea fedha. Ndiyo maana mnawasikia mastaa wetu wa filamu na muziki, kila siku wanalia njaa, wanalalamika kuwa majina yao ni makubwa lakini mapato yao ni finyu. Unajua kwa nini? Ni kwa sababu walikimbia shule.
Ndiyo hao tunasikia wanatumika kubeba unga. Wajanja, wenye shule zao, wanatumia umaarufu wa majina yao kuwapitisha katika viwanja vya ndege kusafirisha mzigo. Nao hawana njia sahihi za kutengeneza maisha yao taratibu kwa kuwa hawana mbinu, wanataka utajiri wa chapchap. Elimu ndiyo mkombozi pekee wa maisha yako!

Post a Comment