Mabadiliko ya tabia nchi duniani
huenda yakaleta madhara makubwa zaidi na ambayo hayawezi kurekebishika,
ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya.
Wanasayansi na maafisa wanaokutana nchini Japan
wamesema ripoti hiyo imefanya uchunguzi wa kina kwa sasa kuhusu athari
za mabadiliko ya tabia nchi duniani.Mifumo asilia kwa sasa haufanyi kazi sawasawa, lakini ongezeko la madhara kwa binadamu ndilo jambo linalohofiwa zaidi.
Afya zetu, makaazi, chakula na usalama vyote viko katika hatari kutokana na kuongezeka kwa viwango vya joto, ripoti hiyo inasema.
Ripoti hiyo ilipitishwa baada ya majadiliano ya kina yaliyodumu kwa wiki moja mjini Yokohama.
BBC SWAHILI
Post a Comment