Vanessa Mdee.
Vanessa Mdee.
Maarufu kama Vee money yeye ni recording artist,
rapper, songwriter, na mtangazaji wa vipindi vya television na
redio,mitandao mengi ya huko nchini Kenya ili ripotiwa kumfananisha
mrembo huyu na mmoja wa wanamuziki wa destiny child,Kelly Rowland.ndiye
msanii anayetoka poa kwenye kila aina ya vazi atakaloamua atupie,unaweza
kudhani kuwa ni model au kwa nini hajawa model nakuchagua kuwa muimbaji
kwa jinsi alivyo tu.
Najma.
Sauti yake na uzuri wake kwa mara ya kwanza kuonekana katika
luninga,ni kwenye video ya tabasamu ya Mr.Blue,ila kutokana na uzuri
wake,naamini asilimia kubwa ya watu huishia kumuangalia Najma tu,naamini
hata asingekuwa na sauti nzuri watu bado wangekuwa wanaangalia video
zake,mbali na uzuri huo yeye pia ni msanii wa bongo fleva na kwa hivi
sasa ana-hit na track yake mpya ya Nimechoka aliyomshirikisha Aslay.
Urembo wake ulijionyesha pamoja na kipaji chake kizuri cha kuimba
pale alipoamua kushiriki mashindano ya Epic Bongo Star Search,ndio
Tanzania ilipoanza kuona uwepo wake,Shaghala baghala ndiye video yake
iliyomuweka kwenye ramani ya bongo fleva mwaka huu,nakufanikiwa kuzidi
kupata umaarufu,uzuri wake unaweza kusema labda amechovya flani hivi.
Jokate.
Ingawa aliweza kuonekana kwenye nyimbo kadhaa za bongo fleva hapo
mwanzo, kupitia uzuri wake akiwa kama model,mwisho wa siku akajaribu
kuweka vocal,zikakubalika,nakushirikishwa kwenye nyimbo mbali mbali
ikiwemo kaka dada.Huyu si tu msanii wa bongo fleva,bali ni Tv presenter
na host katika events mbalimbali,ukiachia mbali u-CEO of Kidoti Lovig co.
Recho
Wengi humfananisha msanii huyu na mkongwe wa muziki wa Bongo fleva
maarufu kama RayC,kuanzia macho,weupe wake,sauti hadi jinsi anavyocheza
unaweza kusema kuwa ni mdogo wake Ray C,ila uzuri wake ndio
uitakaokuweka kwenye luninga yako muda mrefu kumwangalia video
yake,badala yakusikiliza nyimbo.Ni msanii aliyekuja kwa kasi kwenye
Bongo Fleva nakukubalika kirahisi na kubaki on top hadi hii leo,ana-hit
na nyimbo kama Kizunguzungu,upepo,nashukuru umerudi na nyingine nyingi.
Ukiongelea wenye mvuto kwenye sanaa hii ya Bongo fleva,Linah anaweza
kuwa juu ya list,jina lake kamili ni Linah Sanga,anakimbiza sana katika
anga hizi za bongo fleva, kwenye upande mzima wa mvuto,wadau wanasema
kuwa hawezi kulinganishwa na msanii mwingine yeyote.
Source: Vibe Magazine
Post a Comment