0

STAA wa vichekesho anayeigiza sauti za watu mashuhuri nchini, Babu Ayoub ‘Mc Babu Ayoub’ amekutwa na mazito baada ya ukuta wa nyumba yake kuzolewa na mafuriko na kusababisha hasara.

Gari aina ya Toyota Carina la msanii  Babu Ayoub ‘Mc Babu Ayoub’ likiwa limeharibiwa vibaya baada ya kuangukiwa na ukuta
Akizungumza na Amani, Babu Ayoub alisema kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, ambapo ukuta huo uliharibu sehemu kubwa ya gari lake aina ya Toyota Carina alilokuwa ameliegesha nje.
“Mvua ilikuwa kubwa, nikiwa nimelala nilitoka nje baada ya kusikia kishindo.
Gari la Babu Ayoub ‘Mc Babu Ayoub’ likiwa limeharibika vibaya baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyuba
yake
Nikakuta sehemu ya ukuta umeanguka. Nikaamua kurudi ndani kulala. Sikujua kama utazidi kuanguka, lakini cha kushangaza kabla sijapitiwa na usingizi nilishtuka tena kwani kishindo cha pili kilikuwa kikubwa zaidi.
“Mbaya zaidi, sehemu ya ukuta huo uliangukia kwenye chumba ninacholala na kusababisha hasara kubwa ya vitu vya ndani pamoja na kuharibu gari langu kama mnavyoliona (angalia pichani ukurasa wa nyuma wa gazeti hili),” alisema Babu Ayoub kwa majonzi.
Alisema, hasara aliyoipata ukiachana na gari inaweza kumgharimu zaidi ya shilingi 3,000,000 kwani ukuta pekee ulikuwa na matofali 1,200 ambao aliujenga kwa gharama kubwa.
“Hapa nafikiria kuhamia nyumba ya juu ambapo itabidi nitengeneze chumba kimoja kwanza, nimeshauriwa kuhama kwa sababu huu ufa unaweza kusababisha nikapoteza maisha,” alisema Babu Ayoub.

Post a Comment

 
Top