Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchangia kwa kiasi
kikubwa maendeleo ya Wilaya ya Karatu katika Mkoa wa Arusha.
Aidha, chama hicho kimempongeza Rais Kikwete kwa kusambaza maendeleo kwa
Watanzania wote bila kujali msimamo wao wa kisiasa na hata katika maeneo yanayounga
mkono upinzani.
Shukurani na pongezi hizo zimetolewa mchana wa leo, Jumanne, Aprili 22, 2014 na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Mheshimiwa Lazaro Titus Massey
wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la Halmashauri hiyo mjini
Karatu. Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na CHADEMA.
“Ni lazima tutoe shukurani nyingi kwako Mheshimiwa Rais kwa sababu bila wewe kuwa Rais wa
Tanzania sisi Karatu tusingepata jengo hili. Pamoja na kwamba Halmashauri yetu ni HADEMA bado umeamua kuchangia sana maendeleo ya
Wilaya yetu kwa kuchangia kiasi kikubwa ujenzi wa jengo hili. Sisi hata robo ya
fedha za ujenzi huu hatukuweza kuzitoa,” amesema Mheshimiwa Massey
huko kishangiliwa na wananchi. Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu limegharimu kiasi cha shilingi bilioni
1.412 na kati ya hizo, Serikali imetoa shilingi bilioni 1.394 na Halmashauri
imechangia shilingi milioni 18 tu. Akizungumza baada ya kumsikiliza Mheshimiwa Massey, Rais Kikwete amesema kuwa
ni sera ya Serikali yake kusambaza maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali
misimamo yao ya kisiasa wala kuongozwa na hisia nyingine mbali na ukweli kuwa
kila Mtanzania anataka na anayo haki ya kupata maendeleo.
“Sisi hatuna wasiwasi, wananchi wa Karatu wamechagua CHADEMA lakini chama
hiki hakina Serikali.
Wananchi wamechagua chama bila Serikali. Halmashauri
mnayo lakini Serikali tunayo sisi. Katika kusambaza maendeleo, sisi hatuwezi
kubagua. Hiyo ndiyo demokrasia na Serikali yetu inaheshimu sana demokrasia na
misingi ya utawala bora,” amesema Rais Kikwete.
Wakizungumza baadaye kwenye mkutano wa hadhara wabunge wote wawili wa CHADEMA,
waheshimiwa Cecilia Paleso na Israel Nanse wamerudia tena kumpogeza Rais
Kikwete kwa kusambaza maendeleo katika maeneo yote ya Tanzania yakiwemo
yaliyoko chini ya wapinzani.
“Chini ya uongozi wako, maendeleo yamesambazwa na sisi Karatu tumenufaika
sana. Ni matumaini yetu kuwa chini yako, tutaendelea kunufaika na
sera zako sahihi,”amesema Mheshimiwa Paleso.
“Sisi hatuna wasiwasi, wananchi wa Karatu wamechagua CHADEMA lakini chama
hiki hakina Serikali.
Wananchi wamechagua chama bila Serikali. Halmashauri
mnayo lakini Serikali tunayo sisi. Katika kusambaza maendeleo, sisi hatuwezi
kubagua. Hiyo ndiyo demokrasia na Serikali yetu inaheshimu sana demokrasia na
misingi ya utawala bora,” amesema Rais Kikwete.
Post a Comment