Wakati
bunge Maalum la Katiba linaendelea na kikao leo, baadhi ya wajumbe
waliokuwa wanasemekana kuwa ni wanachama wa umoja wa kinachoitwa katiba
ya wananchi (UKAWA) wamejitokeza na baadhi yao kukanusha kuunga mkono
umoja huo.
Mjumbe
wa Bunge la Katiba, Mhe. Ezekiel Oluoch akiingia jana kwenye kikao
cha Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Mhe. Uluoch, ambaye pia ni
naibu katibu mkuu wa Chama cha Walimu (CWT), ni mmoja wa wachangia mada
wakubwa aliyejipatia umaarufu mkubwa mjengoni.Mwenyekiti wa
Bunge Maalum la KAtiba Mhe.Samwel sitta akiliambia Bunge jana kuwa
pamoja na UKAWA kuondoka koramu ya wabunge walio ndani ya ukumbi
imetimia kwa hiyo mchakato wa katiba mpya utaendelea kama kawaida.
Mwenyekiti
wa Kamati namba tano ambaye anatoka chama cha wananchi CUF Mhe.Hamad
Rashid akichangia mjadala jana na kuliaminisha bunge kuwa pamoja na
wanaojiita wana ukawa kutaka mfumo wa serikali tatu yeye anaamini mfumo
wa serikali mbili na kuwashangaa wenzake kwa kuwa vigeugeu na kwamba
maridhiano yatapatikana ndani ya bunge na si nje ya bunge.
Post a Comment