Kibano! Wanawake wawili, wakazi wa jijini Dar wamekumbwa na bonge la
msala baada ya kutiwa mbaroni na kikosi kazi (task force) cha kudhibiti
na kupambana na madawa ya kulevya ‘unga’ ambapo wamekamatwa na mzigo huo
wenye thamani ya mamilioni ya shilingi, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.
Agness Jerad Musaa.
Taarifa zilizodakwa na gazeti hili kutoka ndani ya jeshi la polisi na
kuthibitishwa na kamanda wa kudhibiti madawa hayo nchini, SACP Godfrey
Nzowa zilidai kwamba wanawake hao walikamatwa na madawa hayo kwa nyakati
tofauti katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar hivi karibuni.
Pamela Kihanira.
Kamanda Nzowa alipozungumza na gazeti hili aliwataja waliokamatwa
kuwa ni Agnes Jerald Mussa (42), mkazi wa Magomeni-Mapipa, Dar na Pamela
Kihanira Kibaya (33) (pichani)w, mwenye maskani yake Mbezi-Mwisho,
Dar.
Pamela na Agness wakiwa chini ya ulinzi mkali wa makamanda wa Jeshi la Polisi ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.
Kamanda Nzowa aliweka wazi kwamba Agnes mwenye hati ya kusafiria
(passport) namba AB 624446 ya Februari, 2014, alikamatwa Machi 30, mwaka
huu, mishale saa 8:30 usiku akijiandaa kupanda ndege kuelekea nchini
Uturuki na alikutwa na kilo 1.2 za Cocain zenye thamani ya Sh. milioni
61.5.
Alisema kwamba Pamela mwenye passport namba AB 516016 ya
Aprili 12, 2012, yeye alikamatwa Machi 31, mwaka huu, saa 8.00 usiku
akiwa na kilo 3.5 za Cocain zenye thamani ya Sh. milioni 179.7 akitokea
nchini Brazil.
Kamanda Nzowa aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wa kuwafichua
wahalifu hao na amewataka waendelee kutoa ushirikiano kama huo ili
kudhibiti biashara hiyo haramu.
Habari za uhakika zilisema kuwa baada ya kuhojiwa na polisi, wanawake
hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 2, mwaka
huu ambapo kesi ya Agnes ipo chini ya Hakimu Geni Dudu wakati Pamela
ipo kwa Binge Mashabala.Kesi hizo zilitajwa kusikilizwa tena Aprili 16,
mwaka huu.
Post a Comment