0

BmJyI-oIUAAAE_D

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, makubwa yamkuta follower mmoja wa msanii marufu hapa Tzee Dangote aka Diamond Platnumz, baada ya Diamond kupost picha yake nzuri tu, huku aki-show off tattoo zake, basi ishu ilikuwa ni pale follower huyo alipo muambia Dangote, “sawa umependeza blo,ila sisi watz hatuchoragi hzo v2″, na Dangote Bila kuchelewesha akamshukia na kumjibu “wamakonde vipi?”, hata ukiwa wewe umeandikiwa hivyo hutakuwa na cha kuongezea hapo cause hizo ni tamaduni za watu, tuache wafanye yao.
10296632_388012188006652_2049734321_n
Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipingana kwa vitu mbali mbali wavifanyavyo wasanii wengi hapa bongo, haswa kwenye hili suala la tattoo, wazazi wengi wamekuwa wakiona kama uhuni kuweka tatoo za aina mbali mbali, ila ukweli ni kwamba hata huko nyuma mababu zetu walikuwa wanafanya mambo kama hayo, kwa imani zao tofauti, ila kwa vijana wengi hivi sasa wameonekana kuiga utamaduni wa wenzetu wa nchi za nje, na kusahau hata hapa kwetu nchini kuna makabila yanayochora na kufanya mambo kama hayo.


Post a Comment

 
Top