Hapa mtakua mnafanya makosa.Kabla ya kutafuta mpenzi tulia,tafakari,fanya utafiti,usiwe na pupa wala usongo.
Kumbuka wengi wamepoteza maisha sababu ya mapenzi,wengi wameumizwa sababu ya mapenzi na wengi mapenzi yamewaumiza roho zao.
Mapenzi ni kama viatu,yaani kila mtu ana saizi yake.
Ukipata kiatu kikubwa kuliko mguu wako utasumbuka sana,ukipata kiatu kidogo kuliko mguu wako kitakubana na utateseka sana.Lakini ukibahatika kupata kiatu kinachokutosha hakitakusumbua,hakitakubana,ut afurahi na kuyafurahia maisha.
Katika mapenzi ukimpata mpenzi wa saizi yako,yaani mtu ATAKAEKUFAA na KUKUELEWA kwa kila jambo utayafurahia mapenzi.
Mtu ATAKAEKUFAA maana yake mtu atakaekutosheleza kwa kila kitu kuanzi uchumi,maumbile au viungo vya kimapenzi, vikilingana au vikawa sawa huyo mtatoshelezana na mtafurahiana kimapenzi.
Mtu ukimpata mpenzi mwenye viungo vikubwa kuliko vyako ni karaha, au viungo vidogo kuliko vyako,kwako huyo ni karaha.
Lakini ukimpata mtu wa saizi yako yaani mwenye viungo sawa na vyako utafurahia mapenzi.
Kumbuka kuna watu hasa akina dada waliomba talaka siku ya kwanza tu ya baada ya kufunga ndoa.kumbuka akina kaka siku chache tu baada ya ndoa walianza michepuko.
KUKUELEWA maana yake ni mtu yule tu anayeweza kusoma hisia zako,yaani unataka nini au hutaki nini, kwa wakati gani.
Hapa kuna mambo milioni kidogo.mfano mtu anayeelewa kuwa mpenzi wake anapendelea zaidi chakula gani,nguo gani,kutembelea wapi,afanyiwe nini kitandani au nje ya kitanda,anayeweza kufanya hayo.
Mathalani mpenzi anapenda uwahi kurudi nyumbani au kutoka nae matembezi,kwenda pamoja sokoni,dukani,ibadani,michezon i n.k.Kwa kifupi mtu anyeweza kumsoma mwenza kitabia.
Ukimpata mtu wa hivyo huta ona mapenzi kuwa ni mateso,utaona mapenzi ni matamu kuliko vitamu vyote ulivyowahi kuvitumia na kuvisikia, hapa ndo watu husema,fulani amekua CRAZY..ni mtazamo wangu tu.Aruhusu kukosolewa.
Post a Comment