Mapenzi ni kitu Fulani tofauti sana kwenye hii dunia na hata nje ya hii sayari. Mapenzi kwa kiasi kikubwa sana yanasababisha hata mambo mengine kwenye hii dunia yaende sawa au yaende tofauti hata kama hayahusiani na mahusiano ya mapenzi. Vifo vingi hutokana na mapenzi, kuna magonjwa watu wanaumwa kisa mapenzi, kuna mambo watu wanayafanya si ya kawaida kisa mapenzi.
Ukiachilia mbali PESA, Mapenzi huwa yana nafasi kubwa sana kwenye kitu chochote ndani yahii dunia tunayoishi. Si masikini wala si tajiri, wote kwa pamoja wanahitaji mapenzi kutoka kwa wanaowapenda ili dunia iweze kwenda sawa kwa upande wao. Na ndio sababu hata mimi hapa ninaandika kuhusu mapenzi kwa sababu yananigusa hata mimi na hata wewe unayesoma hapa sasa.
Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele kwako kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.
Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au kutojaliwa kama wewe unavyojali basi hata dunia iwe na raha gani kwako utaiona chungu na hata raha ya maisha hutakuwa nayo hata kama una hela kiasi gani na hata kama una cheo kikubwa kama mfalme au hata rais. Wengine hufikia hatu ya kuteseka tu bila kuondoka kwenye mahusiano kwa kuogopa kuumizwa tena huko waendapo na wengine huondoka baadae sana wakiwa tayari wameshachelewa.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Mojawapo kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;-
1. UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
Kuna vitu vingine hata kudanganyana haileti maana wala haina tija kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.
2. USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa moja. Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.
Kama kuna kitu hukuwahi kumwambia na unahisi ukimwambia atakasirika ni bora umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko aje kugundua mwenyewe itakuwa shida sana kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye mahusiano mwaka wa 4 sasa na kumbe kabla ya kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una watoto 2 kwa huyo mke/mume wa mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza kukuelewa lakini mara nyingi ni kwa shingo upande.
3. ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye love kama kugundua kuwa Yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana mtu mwingine zaidi ya wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa bado wanapenda pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye mapenzi.
Kamwe Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye Ajutie Penzi Lako, Usimfanye Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni Ujanja Lakini Ipo Siku Utahitaji Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata, Laana Ya Mapenzi Ipo, Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi Ya Kweli Yanawezekana Kama Ukiamua na si kwa ku-cheat.
4. DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.
Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri au hata akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo, ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa
Hakuna kitu kinachoweza kumfanya mwenza wako kukukimbia au hata kukosa uaminifu na wewe kama akija kugundua kama wewe ni mropokaji na huna ‘’kifua’’ hasa kwa yale mambo ambayo ni ya chumbani na hayakutakiwa kutoka nje. Hakuna mtu anayependa siri zake kutoka hadharani na huwa inaumiza sana kwenye mapenzi kumpa mtu siri zako then yeye anaenda kusimulia.
Mambo mnayafanya mkiwa wawili tena ndani lakini kesho unaenda mtaani unakuta kila mtu anajua mlichofanya tena wanakuhadithia kama walikuwepo vile, hiyo si kitu nzuri na itakufanya ukimbiwe na kila mpenzi unayempata.
6. TAMAA/KUKOSA UVUMILIVU.
Tamaa ni kitu kingine ambacho hufanya mahusiano mengi kukosa nguvu na mengine kuvurugika kabisa. Kama mpo kwenye mapenzi na mmeamua kupendana kwa shida na raha basi haitakiwi mmoja wenu kuwa na tama na kukosa uvumilivu hata kwa yale mambo yanayoweza kuzuilika.
Kama mpenzi wako ni wa hali Fulani na umeamua kuwa naye basi usiwe na tama kwa vitu vingine ambavyo vinaweza kukusababishia mahusiano yako kukosa nguvu na kufa kabisa. Amini kuwa ipo siku mtakuwa na vitu kama unavyotamani kwa kuongeza bidii kutafuta na kushauriana nini cha kufanya lakini si kwa kutafuta ‘’shotcut’’/njia nyepesi nyepesi zinazoweza kuku-cost hapo baadae.
7. KUKOSA MSIMAMO.
Hii kitu huwakuta wengi sana kwenye mapenzi ya siku hizi. Nadhani ni hali halisi ya dunia ya sasa inachangia pia pamoja na teknolojia tuliyonayo ya kutuwezesha kufanya yale tunayoyaona kwenye mitandao na vyombo mbali mbali vya habari.
Wapenzi wengi siku hizi wamekosa msimamo kwenye mapenzi/mahusiano yao na unakuta tu mmoja anakuwa na wapenzi zaidi ya mmoja na wanakuwa hawafahamiani huku kila mmoja akijua kuwa yeye ndo kila kitu kwa mpenzi wake.
8. KUTOJALI/KUTOKUWA NA MSAADA.
Hii pia kwa kiasi kikubwa inaumiza sana na kupelekea kushuka kwa thamani ya mapenzi miongoni mwa mahusiano mengi haa duniani. Kama kweli unampenda mpenzi wako basi msaidie anapopata matatizo na umjali na kumchukulia kama mpenzi wako na mtu wako wa karibu na sio kukimbia majukumu bila sababu zote za msingi.
Kama huwezi kujali na kusaidia basi usiingie kwenye mahusiano ni bora ukae mwenyewe kuliko kuwepo sehemu usiyotakiwa.
9. UBAHILI.
Huna sababu yoyote ya kuwa na pesa na mpenzi wako akawa anapata tabu kama vile humuoni. Sijasema utoe pesa hata kwa mambo yasiyo na msingi lakini at least utimize majukumu yako kwa mpenzi wako kila unapohitajika.
Kuna vitu vingine hata huhitaji kuambiwa kama unatakiwa kuvishughulikia, ni wewe mwenyewe tu kuwa responsible kumhudumia mpenzi wako. Na hii huwa ina-apply sana kwa wavulana kutokana na kasumba iliyojengeka na mila tulizozikuta.
10. USHOGA/USAGAJI
Hii ipo wazi kabisaaaaaaa…. Hakuna mtu anayependa mtu wake awe Shoga kama ni mvulana au awe Msagaji kama ni msichana. Ni aibu kubwa sana kwa mpenzi wako kuwa katika makundi haya mawili na sidhani kwa akili ya kawaida kama unaweza kufurahia hiki kitu kama utakisikia au kama utakishuhudia kwa macho yako.
Post a Comment