
Seth Bosco.
MSANII wa filamu ambaye ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba, Seth
Bosco amefunguka kuwa
marehemu kaka yake huyo amemchanganya kimaisha
kwani kila kukicha hajui atafanya nini kwa siku nzima.
Seth alisema, tangu Kanumba afariki akiamka asubuhi hajui anafanya
nini kwa siku nzima tofauti na alivyokuwa hai walikuwa wakipanga ratiba
ya siku hata kama wamerudi nyumbani usiku wa manane lazima wapange
ratiba ya siku inayofuata.“Siku hizi nikiamka sielewi nafanya kazi gani kwa siku nzima jambo
ambalo linanifanya nimkumbuke sana Kanumba kwani alipokuwa hai tulikuwa
tukipanga ratiba za siku inayofuata usiku tofauti na sasa,” alisema
Seth.
Post a Comment