MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steve Mengere ‘Steve
Nyerere’ amesema anashindwa kumtathimini msanii wa filamu na muziki
Bongo, Baby Madaha kutokana na kujitenga na wasanii wenzake.
Akifafanua kauli yake, Steve alisema mwanadada huyo anamshangaza sababu hajui yupo kundi lipi kwa kuwa kwenye Bongo Movie hayupo na wala hana kadi ya chama chochote akiwa kama msanii na mbaya zaidi hajitokezi kujumuika na wenzake.
“Hana
kadi ya chama chochote na isitoshe anajitenga na wasanii wenzie,
hahudhurii kwenye shughuli yoyote ile iwe ya huzuni au furaha, kiukweli
simuelewi, abadilike,” alisema Steve.
Paparazi wetu alipomtafuta Baby Madaha kuzungumzia ishu hiyo alisema ana mambo mengi ya kufanya ndiyo maana huwa hashirikiani na wenzake, akipata nafasi atahudhuria.

Post a Comment