Sheikh Abubakar Shariff ‘Makaburi’
anayehusishwa na matukio ya kigaidi nchini Kenya ameuawa jana na watu
wasiojulikana mjini Mombasa.
Sheikh huyo alimiminiwa risasi wakati akiwa katika Gereza la Shimo La Tewa mjini Mombasa jana jioni wakati akisubiri uamuzi wa mahakama kuhusu dhamana kabla ya kuahirishwa kesi yake katika Mahakama ya Shanzu.
Katika tukio hilo, pia mwanafunzi wa chuo aliyetambuliwa kwa jina la Hassih Bayeko aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Walioshuhudia tukio hilo walisema mauaji hayo yalifanywa na watu waliokuwa katika gari jeusi kabla ya kutoweka. Sheikh Makaburi alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuwa mwanachama wa kundi ugaidi la Al Shabaab, lakini alikana madai hayo.
Pia Sheikh Makaburi alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuwaajiri vijana na kuwaingiza katika Kundi la Al Shabaab madai ambayo nayo aliyakana.
Sheikh Makaburi anakuwa muhubiri mkubwa wa tatu kuuawa kwa risasi nchini Kenya ndani ya miaka miwili . Oktoba mwaka jana, mhubiri mwingine Ibrahim Omar aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akitokea kuhubiri.
Pia Julai 2012, Sheikh Aboud Rogo aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye gari. Polisi wameimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mjini Mombasa, huku kukiwa na wasiwasi wa kuzuka kwa vurugu kutokana na mauaji ya Sheikh Kaburi.
Hata hivyo, hadi jana jioni hakukuwa na taarifa zozote za kuzuka vurugu licha ya kwamba hali ya jumla ya mji huo ilikuwa tete.
Taarifa nyingine zilisema kuwa polisi ililazimika kufyatua risasi hewani nje ya kituo cha polisi ambacho mwili wa Makaburi ulipelekwa.
Askari zaidi wametumwa katika mji huo kuimarisha usalama na Ofisi ya Ubalozi wa Uingereza ilitahadharisha kuwa hali ni tete mjini humo.

PATA HABAR ZA UDAKU KWENYE SIMU YAKO
Total Pageviews
26,343,847
PUT YOUR BLOG BELOW FOR
50,000 Tsh MONTHLY.
Other Blogs I Visit
-
-
MACHANGU:WABUNGE WAKATIBA WANALIPA VIZURI - Wasichana wanaofanya biashara ya kujiuza katika maeneo mbalimbali mjini hapa wameelezea neema iliyowafikia kufuatia kujikusanyia pesa ndefu kutoka kwa baa...
-
MAIL CLERK , US EMBASSY - From The Guardian of 2nd April The US Mission in Tanzania provides equal opportunity and fair and equitable treatment in employment to all people with...
-
Wanawake Hufurahishwa na Vitu Vidogo Vidogo Sana Hakuna Haja ya Gharama - Sasa hivi imekua ni kawaida mtu kutumia pesa nyingi labda kumpeleka mpenzi wake kwenye mahotel makubwa au kumnunulia vitu vya thamani ili kumuonyesha mape...
Popular Posts
-
VIDEO:UKWELI WA KUTISHA KUHUSU MALAYA WA UWANJA WA FISI
-
SWALI KWA WADADA...HIVI WANAUME WAREFU NA WEUSI WANA NINI CHA ZIADA KWENYE MAPENZI?
-
JIDE: MIMI NA GARDNER TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA!
-
TAZAMA PICHA HIZI ZINAZOONYESHA TASWIRA YA TRENI ILIYOPINDUKA NA KUUA
-
SAFARI YA DIAMOND KWENDA NIGERIA KUFANYA VIDEO INGINE YAIVA-WEMA AMSINDIKIZA AIRPORT
-
KUNUKA KIKWAPA NA WEUSI KATIKATI YA MAPAJA YANGU VINANINYIMA RAHA
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi....ameeeen
Inna lillah wainnah illayhi rajjiun
Allah anasema " itakapofika nusra ya mwenyezi mungu na kushinda, utawaona watu wanaingia kwenye dini makundi kwa makundi"
Just wait and see