UKITAKA mafanikio lazima uchukue uamuzi mgumu ambao hakuna anayeweza kufikiria kabla.
Kocha huyo atasaini mkataba wa miaka miwili baada ya ule wa miezi sita kufikia tamati. Katika ripoti yake kwa uongozi wa timu hiyo, Logarusic amewaeleza wazi viongozi wake kuwa, ili Simba iwe na ushiriki mzuri msimu ujao wa Ligi Kuu Bara lazima nyota 11 wa timu hiyo waachwe ili wapatikane wengine watakaoisaidia timu kufikia mafanikio.
Kocha wa
Simba, Zdravko Logarusic amesema analazimika kutema wachezaji
wasiopungua 11 ambao ni sawa na kikosi kizima kinachoweza kucheza mechi
ya ushindani. Lengo la Logarusic kufanya hivyo ni ili aweze kujenga upya
timu ya ushindani msimu ujao.
Logarusic
sasa ana uhakika wa kubaki Simba, baada ya kuhakikishiwa na Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Pope kwani awali
hakuwa na uhakika wa kuendelea kubaki katika timu hiyo kutokana na
mkataba wake kumalizika.

Post a Comment