Feri ya Sewol ilipokuwa ikizama.
WAZIRI Mkuu nchini Korea Kusini, Chung Hong Won amejiuzulu kutokana
na vile serikali yake ilivyolichukulia suala la feri iliyozama siku 11
zilizopita.Chung Hong Won amesema kuwa kubaki ofisini ni mzigo mkubwa kwake.
Bwana Chung alizomewa alipozitembelea familia za waathirika katika ajali hiyo ya Sewol, baada ya kuzama katika hali ya kutatanisha.
Takriban watu 200 wanadaiwa kufa maji katika tukio hilo huku zaidi ya mamia wakiwa hawajulikani waliko, wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika ziara ya shule.
Habari: BBC SWAHILI
Post a Comment