Yafuatayo ni yaliyozungumzwa na mjumbe Mh. Zitto Kabwe ambae pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
1.’Nasikitika kwamba mchakato huu ambao ungepaswa kutengeneza maridhiano katika nchi yetu, unajenga chuki, kutengana, majibizano ambayo kwa kweli wananchi wanatushangaa, tumesikia lugha kali sana za kibaguzi humu ndani na hakuna juhudi kutoka viongozi wetu kukemea’
- ‘Hakuna sumu mbaya kwenye nchi yoyote kama kuendekeza ubaguzi, bahati mbaya sana kauli za kibaguzi za vitisho zinatoka watu wanashangilia, watu wanashangilia chuki, wanashangilia matusi.. hatujengi nchi namna hii, tujadiliane kwa hoja na baadae tuamue’
-
‘Muungano ni imani, ama unaunga mkono au hauungi… muundo wowote ule
wa serikali unaweza kuvunja muungano….. iwe moja, serikali mbili au tatu
utavunja tu muungano kama hakuna maridhiano, hakuna muafaka itavunjika
tu, Somalia ilikua nchi moja baada ya kuungana nchi mbili lakini iko
wapi leo? ilikua serikali moja ikavunjika, Ethiopia na Sudan
zimevunjika… hakuna mahusiano yoyote ya idadi ya serikali na kuvunjika
kwa muungano, ni swala zima la maridhiano’
-
‘Huu mchakato ni wa kujenga maridhiano, kuna baadhi ya wajumbe
wanazungumzia gharama kwamba tukibadilisha muundo wa serikali tukawa na
serikali tatu gharama zitakua kubwa sana, hakuna mpaka sasa utafiti
wowote wa kitaalamu ambao unathibitisha hili na baadhi ya wachumi
waliojaribu wameshindwa kulithibitisha sababu unachokifanya ni kunyambua
unaondoa yale mambo ambayo sio ya kidola unayaweka pembeni yanaongozwa’
-
‘Nimesikia kuna watu wanasema tutajenga Ikulu mpya…. kwani nani
kasema lazima tuwe na Marais watatu? tunaweza kuwa na Rais mmoja kwenye
nchi moja na wakuu wawili wa serikali, si tatu hizo… tutahitaji kujenga
Ikulu mpya? ni makubaliano tu
-
‘Tunahitaji kwa ujumla sisi bajeti ya mwaka huu ni Trilioni 18 kati
ya hizo 5.3 ndizo zinazohudumia wizara za muungano, mapato tunayokusanya
ni Trilioni 10 pamoja na mengine ni 11 lakini uwezo wetu ni wa
kukusanya zaidi, kuna jumla ya Trilioni 2.3 hatuzikusanyi kutoka kwenye
makampuni makubwa kila mwaka’
-
‘Uwezo wetu wa ndani wa kodi hivi sasa ni asilimia 17 tu ya pato la
taifa lakini tunao uwezo wa kukusanya zaidi mpaka asilimia 25 ya pato la
taifa, tuna uwezo wa kuendesha muungano wa serikali za idadi yoyote ile
tukiamua wala hatuhitaji kuongeza kodi, tujadiliane tu hatuna sababu ya
kutukanana na kutishana’
-
‘Hofu za serikali ya muungano kutokua na fedha ni hofu halisi wala
msijidanganye sio halisi, ni halisi… ni kweli ushuru wa bidhaa peke yake
hauwezi kutosha kuendesha serikali kwa sababu ushuru wa bidhaa mwaka
jana umetuingizia trilioni 1.9 tu, lakini nini kazi yetu sisi? si ndio
maana tuko hapa? tunaingia humu ndani kwa ajili ya kuboresha hayo
maeneo, kama hatuwezi tumekuja kufanya nini humu ndani?
- ‘Tuhakikishe tunakua na muungano ambao una uwazi, unaeleweka na kila upande unaridhika na niwaambie, tukiwa na muungano ambao upande mmoja sehemu kubwa hauridhiki, gharama zetu za kuulinda huu muungano zitakua kubwa sana ni kama ilivyo muungano ukivunjika, gharama za pande zote mbili kulinda nchi zao ni kubwa zaidi kuliko gharama za muungano wa serikali tatu, manuari za kivita za pande zote kulinda… tuna block ya mafuta namba 8 haijulikani iko wapi, 75% iko Zanzibar 25% iko bara mtafanyaje? mtapigana tu… ndio maana ni lazima tuwe na muungano ambao unaeleweka’
Post a Comment