0

Makubwa! Kaka mkubwa kunako gemu la filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ amefunguka kuwa hana mpango wa kumuoa mwanadada Chuchu Hans kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Vincent Kigosi ‘Ray na Chuchu Hans wakiwa katika pozi.
Akijibu swali aliloulizwa na wanahabari wetu hivi karibuni, kuhusiana na kudaiwa kuwa baada ya mpenzi wake huyo kupewa talaka ana mpango wa kufunga naye ndoa kama ilivyokuwa inadaiwa ambapo alikataa katakata suala la yeye kufunga ndoa na Chuchu.
Diva wa filamu za Kibongo Chuchu Hans.
“Sina mpango wa kuoa ndugu yangu, hayo ni maneno ya watu ambayo yapo tu mitaani ila kwa sasa niko njiani naenda gym baadaye nitakutafuta tuongee.” alisema Ray.
Staa mkubwa kunako gemu la filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa muigizaji huyo kufunguka kuhusiana na suala la ndoa na swali linakuja, je, Chuchu anafahamu kuwa anachezewa tu? Jibu analo mwenyewe moyoni mwake.

Ray na Chuchu katika pozi la mahaba.

Post a Comment

 
Top