0

KICHAPO! Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ amechezea kichapo ‘vitasa’ kutoka kwa bwana’ke aliyetajwa kwa jina la Boniface Matiku ‘Bonny’.

Vai akiugulia maumivu ya kipigo hevi kutoka kwa bwana'ke.
Kwa mujibu wa sosi wetu, ishu hiyo ilijiri hivi karibuni mishale ya usiku nyumbani kwa msanii huyo maeneo ya Mwananyamala-Hospitali jijini Dar baada ya wawili hao kutofautiana.
Ilidaiwa kwamba, Vai akiwa amelala nyumbani alipigiwa simu na Bonny lakini hakupokea ndipo mwanaume huyo akahisi labda alikuwa amechepuka kutoka njia kuu na kwenda kusaliti penzi lao.
Ilielezwa kwamba jamaa huyo alipotimba nyumbani hapo, alimhoji Vai kwa nini alikuwa hapokei simu huku akikutana na meseji za WhatsApp za kumtongoza kutoka kwa mwanaume mwingine ndipo msanii huyo aliyeishi naye kwa kipindi kirefu akamjibu mbovumbovu.
Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ akiwa katika matanuzi.
Chanzo chetu kilidai kuwa mdomo mchafu ulimponza Vai ambaye alipokea kipigo ‘hevi’ hadi akapasuka kichwani lakini haikufahamika alipigwa kwa kutumia kitu gani.
Hata hivyo, duru za kihabari zilidai kuwa timbwili hilo halikuishia ndani kwani wawili hao walitoka nje na kuendeleza mtiti hadi Vai akapoteza ile ‘smart phone’ yake.
Chanzo hicho kilitiririka kwamba baada ya kuona hali inakuwa mbaya huku Vai akitokwa damu, majirani waliwaamulia kisha kumkimbiza Vai hospitalini ambako alishonwa nyuzi kumi kichwani.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa lilimtafuta Vai ambaye alipopatikana alizungumza kwa tabu huku akilalamika maumivu makali.
Vai akiwa na bandeji kichwani baada ya kichapo.
“Ni kweli Bonny amenipiga sana sijiwezi,” alisema Vai ambaye anatarajia kusukuma sokoni filamu yake ya Beautiful Liar.
Alipoulizwa chanzo cha ugomvi na kama Bonny amechukuliwa hatua gani, Vai alisema: “Ni wivu wa mapenzi. Bonny ana wivu sana. Sijamchukulia hatua yoyote kwani nampenda sana Bonny. Pia ameniomba msamaha na ananihudumia hivyo nimemsamehe.”
Hivi karibu Vai aliripotiwa na gazeti hili baada ya kunaswa kwenye mtego wa kujiuza wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ndipo mgogoro na Bonny ulipoanza.

Post a Comment

 
Top