Itakumbukwa kuwa, Diamond ndiye msanii aliyewahi kumpa zawadi ya gari marehemu Gurumo kutokana na kuguswa na mchango wake katika tasnia ya muziki nchini.
Diamond akimsaidia mzee Gurumo kupanda stejini kabla ya kumkabidhi gari Agosti 29, 2013.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kitendo cha Diamond kutoonekana katika
mazishi hayo ni kama amejishushia heshima kubwa aliyojijengea pale
alipomthamini marehemu huyo kwa kumpa gari aina ya Toyota FunCargo.“Tulitegemea tungemuona msibani lakini kwa kutokuwepo kwake ni kama mchango wake wa kumpa gari Gurumo hauna maana,” alisema shuhuda mmoja aliyekuwepo msibani hapo.
Mapaparazi wetu walidamka asubuhi hadi nyumbani kwa marehemu Gurumo na kujumuika na waombolezaji.
Breki ya kwanza kwa mapaparazi wetu ilikuwa nyumbani kwa Diamond Sinza-Mori jijini Dar ambako hawakumkuta.
Mapaparazi hawakuchoka, wakahamishia ‘majeshi’ nyumbani kwa mwanandani wake Wema, Makumbusho, Dar ambako mlinzi alibainisha kuwa, Diamond yupo na ‘bebi’ wake Wema.
Waandishi wetu walimvutia waya Diamond lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Kusaka data zaidi, mapaparazi wetu walimtafuta meneja wa msanii huyo, Babu Tale ambaye alidai kuwa eti Diamond alikuwepo msibani Mabibo lakini hakwenda Kisarawe ambako mazishi yalifanyika.
Mzee Gurumo akionyesha ufunguo wa gari alilozawadiwa na Diamond.
“Tulikuwepo nyumbani kwa marehemu. Nilikuwa mimi na Diamond tena
tumefika muda huohuo ndiyo mwili ukawa unapelekwa kwenye gari. Huwezi
amini tulijumuika kuupandisha mwili kwenye gari na sisi tukarudi
nyumbani kuendelea na shughuli zetu,” alisema Babu Tale.Mapaparazi wetu baada ya kutoshibishwa na maelezo hayo, juzi Jumatano walimtwangia simu Diamond ambaye alizungumza kwa ‘kujikanyagakanyaga’.
Mapaparazi wa Global walikuwa jirani na gari alilotaja Diamond lakini hawakumuona staa huyo achilia mbali waombolezaji wengine ambao waliuliza kwa nini msanii huyo hakufika kwenye msiba wa rafiki yake mkubwa!
Post a Comment