Mnenguaji maarufu Bongo aliyewahi kutopea kwenye matumizi ya madawa
ya kulevya kabla ya hivi karibuni kuamua kuacha, amegandwa na skendo ya
kuiba siku lakini mwenyewe alipoulizwa, alishangazwa na madai hayo huku
akidai kuwa hawezi kufikia hatua hiyo.Awali chanzo chetu kilitunyetishia kwamba, mdada huyo alizama kwenye
saluni moja iliyopo Kijitonyama na kuweka fresh nywele zake lakini
alipotoka tu mmoja wa wateja akalia kuibiwa simu yake.
Kwa kuwa yeye ndiye aliyetoka muda ule watu wakajua ndiye
aliyechukua, walipotoka kumuangalia ili wamuulize alikuwa
ameshatokomea,” alidai mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Mwandishi wetu alipozungumza na Aisha kuhusu ishu hiyo alisema:
“Niibe simu, mh! Kweli ninaishi mitaa hiyo na mara mojamoja nikitoka
kazini nimechelewa naendaga saluni lakini sijawahi kusikia wala kuitwa
na mtu akidai nimeiba simu. Hao wanaonisema hivyo watakuwa na sababu zao nyingine tu za kutaka kunichafulia jina langu.”
GPL
Post a Comment