0

MSANII mkongwe kunako gemu la filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kuwa hawezi kuachika kwenye ndoa yake iliyodumu kwa miaka 13 na wanaosubiri aachwe, watasubiri sana.

Msanii mkongwe kunako gemu la filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’.
Akizungumza na paparazi wetu juzi Cathy alisema kuwa, amekuwa akizushiwa kwamba anatoka nje ya ndoa na wasanii tofauti lakini hayo ni maneno tu ambayo hayamuumizi mumewe kwani ni muelewa na hawezi kuyasikiliza.
“Ndoa yetu ina miaka 13 sasa, nawashangaa sana wanaosema mimi nachepuka kwa kutoka na Dude, ninachoweza kusema ni kwamba hata wakimwambia mume wangu hawezi kuniacha maana mimi na yeye tulianzia mbali sana, kusikiliza umbeya wa watu ni kupoteza muda,” alisema Cathy.

Post a Comment

 
Top