0

STAA wa filamu za Kibongo, Aisha Bui amepata mtoto wa kike aliyejifungua kwa njia ya upasuaji lakini kumekuwa na usiri mkubwa katika jambo hilo.

Staa wa filamu za Kibongo, Aisha Bui.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Aisha alisema anamshukuru Mungu kwa kumjaalia mtoto wa kike aliyempa jina la Saloma.
“Nimefurahi sana, kumpata mtoto ni jambo la kumshukuru Mungu na sasa najisikia raha sana kuitwa mama,” alisema Aisha na kuongeza kuwa, mwanaume aliyezaa naye ni mchumba wake wa siku nyingi ambaye anaishi nje ya nchi na wanatarajia kufunga ndoa siku si nyingi.

Post a Comment

 
Top