Kuna mambo fulani madogo huwa tunakosea sana tunapokuwa kwenye mapenzi
labda pengine ni kutofahamu au labda hata ni makusudi. Kuna mambo
tunayafanya ambayo bila kujua huleta matokeo ambayo hatuja ya tarajia
upande wa pili kwa wenza wetu. haya hapa:
1) Ili mweza wako atulie hakikisha unajua nini hapendi: yani ni hivi
hakikisha kitu ambacho hutaki akufanyie vilivile na wewe usifanye kitu
ambacho hapendi
2) Uongo: uongo ni mbaya sana kwani unapomdanga mara kwa mara na
kigundua anaweza kupoteza uaminifu kwako na pia inaweza kumfanya
asitulie atoke nje, kutafuta njia mbadala
3) Mwache ajisikie na yeye ameshinda wakati mwengine, kwa mfano mkiwa
mnabishana kitu au kugombana jaribu kuwa mdogo ili ajione na yeye ni
mshindi, ila usifanye hivyo mara zote kwani atazoea.
4) Penda sana ndugu zake, pia jichanganye kwenye mahafali ya kifamilia, misiba hata harusi muenyeshe.
5) Muulize nini anataka haswa mkiwa kwenye kufanya mapenzi, muulize usiogope kuwa huru kabisa
6) Usimuite jina lake mpe jina lingine la kimapenzi, wala sio bby au swt
kwani yameshazoeleka sana na pia labda ameshaitwa sana hayo majina,
tafuta hata lingine kama Mumy, My lady, princess na mengine mengi
mazuri.
7) Mtoe out siku moja moja, nenda nae dinner au hata ice creem
8) Na kingine Mkumbushe Kusali kila mara kabla ya kulala na kuamka
Kazi kwako fanya hayo utapata majibu
Post a Comment