Drake anasema ‘We started from the Bottom’ lakini Mweusi Nick wa Pili anasema ‘Haikuwa Rahisi’.
Nick wa Pili ambaye ni moja kati ya rappers bora zaidi Tanzania na
mshindi wa tuzo ya KTMA ameelezea jinsi alivyohangaika wakati akiwa
shule ya msingi katika maisha ya kawaida ambayo wapo watanzania wengi
wanayoyaishi hadi hivi sasa.
Akizungumza katika kipindi cha The Jump Off ambapo yeye ndiye Mkali
wa The Jump Off wa Wiki hii anayesimulia story ya maisha yake ambayo ni
somo tosha kwa vijana ambao wanahangaika kutafuta, rapper huyo ameeleza
jinsi alivyofanya shughuli ya kuuza sambusa akiwa darasa la tatu hadi
darasa la saba kila anapotoka shuleni saa nne usiku huku akiwasaka
wateja kokote walipo..
“Mimi maisha yangu niliyopitia unajua sio kama watu
wanavyonidhania, mimi nimepitia a very hard life. Mimi kuanzia nikiwa
darasa la tatu nilikuwa nauza sambusa.
"Nilikuwa natembeza kwenye nyumba
za gongo, banana, mabaa na nilikuwa nauza kuanzia saa kumi hadi saa nne
usiku, niko darasa la tatu nimeuza mpaka darasa la saba.
"Kwa hiyo watu
wanapotuona Nick wa Pili… it’s not easy. Nafikiri kama ukipata
kusikiliza albam ya Chindo kuna ngoma inaitwa ‘Haikuwa Rahisi’
nilijaribu kuweka historia yangu pale..ilikuwa ngumu.”
Nick wa Pili ambaye ni mdogo wake Joh Makini, ameeleza kuwa hata
alipomaliza darasa la saba kuingia sekondari ilikuwa ngumu kutokana na
kikwazo cha fedha.
Ilimbidi akae nyumbani miezi miwili akitafuta shilingi 20,000 za
karo. Bahati nzuri rapper huyo alizipata fedha hizo na alipoingia shule
alikuta tangazo la mtihani wa kumaliza muhula na alipoufanya alishika
nafasi ya pili kutoka mwisho.
Kutokata tamaa na kukaza ndiko kumempa nafasi ya kung’aa na kupata
shahada ya uzamili (masters) na kufanya vizuri kwenye muziki hadi sasa.
“Kwa hiyo ndio life tuliyopitia, lakini if you put a struggle in everything…it’s possible.”
Nick anaachia wimbo wake alioupa jina la ‘Staki Kazi’ akiwa amewashirikisha G-Nako na Ben Pol.
Credit: Times 100.5 FM
Post a Comment