KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema ‘ndoa’ upinzani bungeni iliyozaa Baraza Kivuli la Mawaziri la vyama vya Chedema, CUF na NCCR-Mageuzi, ni mwendelezo wa ubabaishaji na matusi makubwa kwa vyama vingine vilivyokubali ndoa hiyo hasa CUF.
Nape amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Parking mjini Nzega na kusema kuwa mwenendo huo wa vyama vya upizani, utasambaratisha na kuua vyama vya upizani nchini.
Akinukuu taarifa rasmi za Bunge zilizomkariri Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), Nape alisema ameshangazwa na pande zote mbili za ndoa ya Chadema na CUF.
“Ngoja ninukuu baadhi ya maneno ya kejeli na matusi kutoka kwa Tundu Lissu kwa vyama vya upizani vilivyopo bungeni ili kuthibitisha unafiki mkubwa wa wapizani wanchi hii. “Na hili nimeamua kulisema baada ya waandishi wengi kutaka kujua kauli yangu juu ya Baraza Kivuli la Mawaziri lilitangazwa na Mbowe (Freeman, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni) hivi karibuni,” alisema Nape huku wananchi wa Nzega wakimshangilia kwa makofi na vigelele.
Nape alisema matusi aliyotukana Lissu bungeni dhidi ya vyama vya upinzani vyenye wabunge bungeni, hayavumiliki na ni ajabu kuwa pande zote za ndoa ya vyama vya upinzani bungeni wamesahau.
“Tundu Lissu alihoji bungeni kuwa inawezekanaje kuunda Kambi moja Rasmi ya Upinzani bungeni wakati vyama vina Katiba tofauti, kanuni tofauti na taratibu tofauti za kuendesha mambo yake,” alisema Nape na kuongeza kuwa inawezakanaje Kiongozi huyu wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani bungeni, akasimamia nidhamu kwa muungano wa namna hii?
“Leo kimetokea nini kilichombadilisha Lissu na Chama chake kama sio unafiki? Ni lini walibadili Katiba, Kanuni na taratibu kabla hawajaunda mseto wao? “Akawakejeli sana CUF na kujiapiza kuwa Chadema haitakubali kuwa na ndoa na Chama chenye ndoa nyingine… sasa hiyo ndoa ya kwanza imekufa lini?” Alihoji Nape.
Post a Comment